Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameagiza soko la mnada wa Upili eneo la Mtyangimbole Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma likabidhiwe Halmashuri ya Madaba.
Waziri Mpina ametoa agizo hilo baada ya kutembelea na kukagua mnada huo katika ziara ya kikazi wilayani Songea.
Mpina ameziagiza Halmashauri za songea na madaba kukabidhiana soko hilo haraka ili serikali iweze kuendelea na taratibu za ukarabati wa soko hilo ILI liweze kuingiza mapato ya serikali.
“Naagiza makabidhiano yafanyike haraka ili Halmashauri inayo husika na uendeshaji wa soko hilo ifanye utekelezaji wake na maduhuli ya serikali yakusanywe kulingana na sheria za Nchi’’,amesisitiza Mpina.
Aidha ametaka ukarabati ufanyike mara moja na kuajiri mlinzi wa muda atakayehusika na kulinda usalama wa eneo hilo na kuhakikisha mnada unafanyika ndani na siyo nje ya jengo kama ilivyo sasa hivi sasa ambapo mnada huo umekuwa uikiingizia kiasi cha wastani wa shilingi milioni 18 kwa mwaka.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema soko la mnada la Mtyangimbole lilikuwa likimilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Songea kabla ya Halmashauri hizo kugawanywa mwaka 2014 na uendeshaji wake kufanywa na Halmashauri ya wilaya ya Songea huku maduhuli yakikusanywa na Halmashuri ya Madaba.
Wadau wameishukuru serikali kwa maamuzi hayo na ukarabati ambao utaboresha mazingira ya kutolea huduma na kuimarisha biashara kwa sababu mazingira bora na mazuri humvutia mteja kuja kupata huduma bora.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa