Leo ni Jumamosi ya mwisho wa mwezi siku maalum ya usafi wa mazingira kitaifa ambapo katika Manispaa ya Songea imefanyika Mtaa wa Mjimwema B eneo ambalo utafanyika mkesha wa Mwenge wa Uhuru Juni 7 mwaka huu.Watazame wananchi wa Kata ya Mjimwema Manispaa ya Songea walivyojitokeza kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi Mei 2018.Usafi umefanyika Mtaa wa Miimwema B eneo ambalo pia yatafanyika maadhimisho ya kilele cha siku ya mazingira duniani kimkoa Juni 5 mwaka huu mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme.Eneo hilo la soko la Mtaa wa Mjimwema B ,ni eneo ambalo utafanyika mkesha wa Mwenge wa Uhuru Juni 7 mwaka huu katika Manispaa ya Songea.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa