MANISPAA ya Songea imebahatika kuwa na vivutio adimu vya utalii ambavyo vimekuwa vinawashangaza wengi wanaotembelea vivutio hivyo.Moja ya vivutio hivyo ni chanzo cha mto Ruvuma ambao unamwaga maji yake Bahari ya Hindi. Chanzo hiki kipo katika Hifadhi ya misitu ya milima ya Matogoro katika Manispaa ya Songea iliyoanźishwa miaka ya 1950. Milima hii pia ni chanzo cha Mto Luhira ambao unatengeneza mto Ruhuhu unaomwaga maji ziwa Nyasa na mto Luegu ambao unaungana na mto Rufiji na kumwaga maji bahari ya Hindi.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa