Picha za matukio mbalimbali ya viongozi wa Serikali, chama, na Wenyeviti wa Mitaa pamoja na Wajumbe wake wakipewa kiapo cha uadilifu na utii kilichotolewa leo tarehe 29 Novemba katika Ukumbi wa wa shule ya Sekondari ya Wasichana Songea kwa lengo la kuwaapisha viongozi hao ambao wamepata ushindi wa kishindo baada ya kufanya uchaguzi wa kupata viongozi hao ambao ulifanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea alisema katika uchaguzi uliofanyika katika mitaa 94 iliyotangazwa na TAMISEMI ambapo matokeo ni CCM wameshinda kwa nafasi zote z Wenyeviti, Wajumbe mchanganyiko ,pamoja wajumbe kundi la Wanawake.
Kiapo hicho kimetolewa chini ya Hakimu Happines Shelembi Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mfawidhi ya Songea.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa