Mwenyekiti UWT Taifa Mary Chatanda amewataka wananchi kulinda maadili na utamaduni kwa watoto na jamii kwa ujumla na kuepuka matendo yasiyofaa ambayo yanaathiri jamii na kizazi kijacho.
Alisema “kuna tabia ambayo hujitokeza kwa baadhi ya wanawake ambao huvaa gauni kwenye sherehe lilnalotambulika kama kijora kisha kujimwagia maji mwilini na kucheza bila stara (VIGODORO) kitendo ambacho kinavunja maadili ya kitanzania.”
Ametoa wito kwa Serikali za Mitaa, Vijiji na vitongoji, Jeshi la Polis, pamoja na uongozi ngazi ya Wilaya kuhakikisha wanadhibiti matukio yoyote yenye viashiria vya uvunjifu wa maadili na tamaduni zetu wanatakiwa kukamatwa mara moja ili kudhibiti matukio hayo.”alisisitiza”
Matukio ya Ubakaji, Ushoga, ukatili wa kijinsia, uvutaji wa madawa ya kulevya, ukeketaji pamoja na manyanyaso ya kijinsia hayakubaliki katika ardhi ya Tanzania na endapo itajitokeza matukio kama hayo yachukuliwe hatua za kisheria mara moja.
Hayo yamejiri wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda iliyofanyika kwa siku moja tarehe 29 Julai 2023 ambapo alifanikiwa kutembelea mradi wa ujenzi wa Hosptali ya Wilaya ya Songea, Kuweka jiwe la Msingi katika nyumba ya Katibu wa CCM Wilaya, kutembelea uwanja wa ndege, pamoja na kuongea na wananchi katika viwanja vya Lizaboni kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Bi Chatanda aliongeza kuwa lengo la Ziara hiyo ni kuhamasisha wanachama kujiunga na CCM, kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kutoa taarifa kwa jamii juu ya utekelezaji wa shuhuli za miradi.
Akitoa pongezi mradi wa ujenzi wa Hosptali ya Manispaa ya Songea alisema “ Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani ameendelea kusimiamia Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambapo katika Idara ya Afya kwa Manispaa ya Songea ameweza kutoa fedha zaidi ya Bil. 4 ambazo zimejenga vituo vya afya 4 na hosptali ya Wilaya ambayo ipo hatua ya ukamilishaji. “alipongeza”
Kwa upande wake Dkt. Damas Ndumbaro (MB) Waziri wa Katiba na Sheria alisema kabla ya uongozi wake Manispaa ya Songea ilikuwa na kituo cha afya 1 lakini hadi hivi sasa Manispaaa ya Songea ina vituo vya afya vinne na Hospital 1 moja ambayo inaendelea kujengwa na itaanza kutoa huduma za awali OPD ifikapo tarehe 01 Agost 2023.
Dkt. Ndumbaro alisema, anaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha za miradi ya maendeleo hususani katika sekta ya Barabara, Elimu, Afya, Maji pamoja na Ruzuku ya Mbolea kwa Wakulima.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa