Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael amewataka Waheshimiwa Madiwani na wataalamu kushirikiana katika kutekeleza na kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo ili kuleta mafanikio.
Hayo yamejili katika mkutano wa baraza la kwanza la Madiwani lililofanyika tarehe 03 Novemba 2022 kwa lengo la kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi wa miradi yamaendeleo katika kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka 2022, pamoja na taarifa ya mapato na matumizi ya kipindi cha julai hadi septemba 2022.
Baraza hilo lilianza kwa kupokea maswali ya papo kwa papo yaliyoulizwa na waheshimiwa madiwani katika mkutano na kutolewa ufafanuzi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea kuhusu changamoto mbalimbali za miundombinu ya shule, ujenzi wa Soko la Manzese na utoaji wa vibali vya sherehe kwenye jamii.
Mhe. Mbano alisema Manispaa ya Songea inatoa shukrani kwa Serikali ya wamu ya sita kwa kutoa fedha Bil. 1.52 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 76 ambayo ya meanza kujengwa na yatakabidhiwa ngazi ya Wilaya tarehe 30 Novemba 2022, Hivyo ametoa rai kwa wataalamu na Waheshimiwa Madiwani kuongeza jitihada katika kusimamia ujenzi wa madarasa ili kufikia lengo ya Serikali yaliyokusudiwa.
Akitoa ufafanuzi Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko ambapo alisema “ Manispaa ya Songea kuanzia mwezi novemba 2022 itatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya kumpata mkandarasi ambaye atafanya kazi ya kujenga miradi mbalimbali ikiwemo na ujenzi wa miundombinu ya barabara na ya soko pamoja na ujenzi wa viwanda katika eneo la Lilambo.”
Dkt. Sagamiko aliongeza Elimu ya utoaji wa vibali vya sherehe imetolewa kwa wananchi kupitia maafisa watendaji wa kata ambapo agizo hilo linaendelea kutekelezwa kwa kulipia kiasi cha shilingi elfu hamsini 50,000 kwa kila sherehe na kukatiwa risiti halali.
Alisema kuanzia julai hadi septemba 2022 Manispaa ya Songea ilipokea na kukusanya kiasi cha shilingi Bil 12,197,783,320.46 ikiwa ni mapato ya ndani pamoja na ruzuku kutoka Serikali kuu.
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa