Kamati ya lishe Manispaa ya Songea ikiongozwa na Afisa Elimu Sekondari Freck Sichalwe kwa niaba ya Mkurugenzi imeweka utaratibu wa kutoa Elimu ya afya na lishe kwa vitendo kwa wazazi wenye watoto chini ya miaka 5 ikiwa na lengo la kuondoa utapiamlo na udumavu.
Amewataka wazazi na walezi kuzingatia kutumia chakula chenye viini lishe kwa Mama mjamzito ili kusaidia maendeleo ya ukuaji ya mtoto.
Alisema Wazazi wanatakiwa kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka ili kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafuzi wa mazingira yakiwemo malaria, mafua, kuhara pamoja na kipindupindu ambapo usababisha kupoteza nguvu kazi ya Taifa.Sichalwe alibainisha
Hayo yalijili tarehe 21 machi katika siku ya afya na lishe ya kijiji ambayo hufanyika kila robo moja ya mwaka ambapo kwa Manispaa ya Songea zoezi hilo lilifanyika mtaa wa Likuyufusi kata ya Lilambo Manispaa ya Songea.
Kwa upande wake Afisa Lishe Manispaa ya Songea Alberth Semkamba Ametoa rai kwa jamii kuzingatia umuhimu wa siku 1000 za mwanzo za mtoto kuanzia utungaji mimba hadi kuzaliwa kwa mtoto atatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya Mama pekee hadi pale tu atakapofikisha umri wa miezi 6.
Kwa upande wa wazazi walisema “Tunaishukuru Serikali kwa kutoa Elimu hii ya afya na lishe katika mtaa wa Likuyufusi kwani hii itasaidia kutoa malezi bora kwa watoto na kuondokana na changangamoto zinazojitokeza kwa Mama mjamzito na mara baada ya kujifungua kwa kuzingatia maelekezo ya watalaamu wa afya juu ya lishe bora”. “Wazazi walibainisha.”
“LISHE BORA KWA AFYA NA MAENDELEO KWA KIZAZI KIJACHO”
Imeandaliwa na;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa