Mhazina wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania (TALGWU) ngazi ya Taifa Siston Mizengo ametoa maagizo kwa viongozi wa TALGWU Mkoa wa Ruvuma kusajili wanachama wapya katika chama hicho ambacho kilifanyika tarehe 27 Aprili 2021 katika ukumbi wa deport (Angaza) Songea Mjini.
Akitoa maagizo hayo wakati akifanya ziara katika Mkoa wa Ruvuma, Manispaa ya Songea Mizengo alisema ni wajibu wa kila kiongozi kuhahakisha anaongeza wanachama wapya wa TALGWU katika tawi lake ili kuongeza mapato ambayo yatasaidia kuendesha shughuli mbalimbali za chama.
Licha ya agizo hilo amewataka viongozi kuhakikisha wanatumia vizuri fedha za chama katika tawi husika, pia aliahidi kubeba changamoto zinazowakabili wanachama wa TALGWU Mkoa wa Ruvuma na kuziwasilisha katika ngazi ya juu (Taifa) ili kupata utatuzi wa changamoto hizo.
Hadi sasa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania (TALGWU) kimefanikiwa kununua magari 14 kwa ajili ya matumizi ya chama ambapo Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mkoa ambao kuletewa gari moja. ‘Mizengo Alibainisha’.
TALGWU BANDO – MPANGO MZIMA,
CHAMA IMARA HUDUMA BORA KWA WANACHAMA.
IMEANDALIWA NA,
AFISA HABARI MANISPAA,
AMINA PILLY.
06.05.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa