Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
13 JUNI 2022
Baraza la habari Tanzania (Media Council of Tanzania - MCT) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mawakili Afrika Mashariki ( East Africa Law Society - EALS) wametoa mafunzo kwa waandishi wa habari na Maafisa Habari, mawasiliano na Uhusiano Serikalini kwa lengo la kujadili kuhusu sheria ya haki ya kupata taarifa ya mwaka 2016 yaliyotolewa tarehe 11 Juni 2022 jijini Mbeya.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya mawakili Afrika Mashariki, Wakili David Sigano alisema kuwa mafunzo hayo yamelenga kutoa elimu juu ya uhuru wa kujieleza kwa waandishi wa habari, dhana ya vyombo vya habari kwa jamii pamoja na uhuru wa vyombo vya habari kwa kuzingatia sheria na kanuni za uandishi kulingana na Sera ya habari nchini Tanzania.
Amewataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa uadilifu na kushiriki katika kufanya mazoezi bora ya kimataifa katika kushikilia uhuru wa kujieleza pamoja na namna bora ya uandishi wa habari za kiuchunguzi, habari za utamaduni wa kimataifa pamoja na mabadiliko ya sheria mbalimbali za uandishi wa habari.
Wakili Sigano aliongeza kuwa uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu katika kulinda haki za binadamu kwa kutoa haki ya kupokea taarifa pamoja na haki ya kutoa taarifa kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari.
Naye Paul Malimbo (Media Monitaring and Press freedom Violation Tanzania) amewataka waandishi wa habari kuunga mkono shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Serikali katika jamii ikiwemo na kuandika habari zinazohusiana na zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu ili kusaidia wananchi kuwa na uelewa na kushiriki katika zoezi hilo kikamilifu.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa