Tarehe 14 Oktoba 2024 ni siku ya maadhimisho ya Hayati Mwl. Julius Kambambarage Nyerere ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe hiyo ambapo kwa Manispaa ya Songea maadhimisho hayo yamefanyika kwa kufanya mazoezi ya viungo na michezo mbalimbali.
Katibu Tawala Mtella Mwampamba amesema “ Tumuenzi Mwalimu Julius Nyerere kwa matendo mema aliyokuwa ameyafanya ambayo yamepeleakea leo Watanzania kuwa huru na kuendelea kushikamana katikakulijenga Taifa letu.”
Alisema Mchakato wa uchaguzi upo ngazi ya msingi ambao tunaendelea na mchakato wa kujiandikisha kwenye orodha ya Wapiga kura ambapo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kwenda kujiandikisha ili kupata haki ya kuchagua na kuchaguliwa ambapo zoezi hilo limeanza tarrehe 11 hadi 20 Oktoba 2024.
Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi Wakili Bashir Muhoja amemtaka afisa michezo kuratibu zoezi la michezo kwa watumishi wa Manispaa ili kuweza kuimarisha afya za watumishi.
Alisema Zoezi hili limefanyika kwa lengo la kuhamashisha wananchi kwenda kujiandikisha ambapo limeanza tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024 huku akibainisha tayari watu 36,000 wamejiandikisha kati ya wanachi 170,000 ambao wanatakiwa kujiandikisha katika Manispaa ya Songea.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILAIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa