PICHANI ni Nduna Songea Mbano Luwafu, alipigwa picha hii muda mfupi kabla ya kunyongwa na wajerumani Machi mwaka 1906.Mashujaa wengine 66 wa Majimaji walinyongwa Februari 27,1906.
Songea Mbano alinyongwa pekee yake siku tatu baada ya wenzake 66 kunyongwa na kuzikwa katika kaburi la pamoja àmbalo lipo katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea. Hata hivyo Songea Mbano alizikwa katika kaburi la pekee yake.Inasadikika wajerumani walikata kichwa chake na kuondoka nacho na hapa wamezika kiwiliwili chake.
Wazee wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea kila mwaka wamekuwa wanaiomba serikali na Wizara ya Maliasili na utalii kufuatilia kichwa cha Songea nchini Ujerumani. Kwa ajili ya kumuenzi shujaa huyu mji wa Songea na wilaya ya Songea imetokana na jina lake shujaa huyu ambaye wajerumani hawatamsahau.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa