Siku ya Wajane Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 23 Juni kila mwaka baada ya Umoja wa Mataifa kupitisha siku hii kuwa ya kimataifa kupitia Azimio Na. A/RES/65/189 la tarehe 21 Desemba 2010 na ilianzishwa na kuasisiwa na Lord Loomba mwaka 2005.
Kutokana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wajane wanachama wa Umoja wa kimataifa waliazimia kuadhimisha siku hii kwa lengo la kuongeza uhamasishaji wa kupinga ukiukaji wa haki za binadamu kwa wajane.
Akizungumza Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Ruvuma Xsaveria A.Mlimira amewataka maafisa ustawi wa jamii na maafisa watendaji kata/mitaa kuendelea kuelimisha jamii juu ya ugawaji wa mirathi kuzingatia kanuni na sheria ili kuleta usawa na haki ikiwemo haki ya kuwalea watoto, haki ya kumiliki Ardhi pamoja na mali.
Hayo yamejili katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wajane Duniani ambayo yamefanyika leo tarehe 23 Juni katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kuudhuriwa na viongozi wa Dini, Watalaamu pamoja na wananchi ambapo yakiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano na kutatua changamoto katika jamii.
Kupitia sanse ya watu na makazi ya mwaka 2023 Tanzania ina jumla ya wajane 1,396,262 ambapo serikali imefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kuanzishwa kwa kampeni ya “maadili yetu Taifa letu” kwa lengo la kuwatunza na kuwalinda wajane, kuanzishwa madawati ya jinsia na watoto 573 katika vituo vya Jeshi la Polisi na Magereza kwa lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia wakiwemo wajane pamoja na kuundwa kwa Wizara mahsusi ya Maendeleo ya Jamii,jinsia,wanawake na makundi maalum.Alisem
Kwa upande wake Afisa Dawati la jinsia na watoto Songea Sajenti Paulina ametoa rai kwa wajane kutoa taarifa kwa wakati ili kupata msaada wa kisheria pale ambapo wanakutana na changamoto ikiwemo kunyanyashwa na kunyimwa haki ya umiliki wa mali.
Wametoa shukrani za dhati kwa serikali ya awamu ya sita kwa kuwatambua na kuwajali wajane kwa kuweka mifumo ya kulinda haki na kuongeza huduma za msaada wa kisheria Na: 1ya mwaka 2017.Wananchi Walishukuru
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa