Mkuu wa Mkoa Ruvuma Kanal. Laban Thomas amewataka viongozi,wazazi au walezi pamoja na wadau mbalimbali kupinga na kukemeea vitendo vya vinavyoashiria ukatili wa kijinsia ikiwemo na ndoa ya jinsia moja .
Amesema Wazazi wanapaswa kutoa malezi bora kwa watoto wao kwa kuwapatia elimu kimazingira na madhara ya kushiriki ndoa ya jinsia moja ili kulinda vizazi vya sasa na vijavyo.
Hayo yalitamkwa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Nyasa kwa lengo la kuwakumbuka wanawake 15000 walioandamana kwa lengo la kudai haki na Ujira ambayo huongeza chachu kwa wanawake katika kudai haki na usawa katika jinsia.
,Kanal. Laban ametoa rai kwa wananchi kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) kwa kujitokeza kupima afya mara kwa mara ili kujilinda na maradhi na jamii kwa ujumla.
Alilibainisha, kuwa takwimu za maambukizi ya Virus vya Ukimwi kitaifa ni 4.7%, katika Mkoa wa Ruvuma ni 5.6%, ambapo halmashauri ya Madaba ni 10.4%, halmashauri ya Mbinga DC 4.8%, halmashauri ya Mbinga Mji ni 7.8%, halmashauri ya Namtumbo ni 4%, halmashauri ya Nyasa ni 5.4%, halmashauri ya Songea DC ni 6.2, halmashauri Manispaa ya Songea ni 10.5% na halmashauri ya tunduru ni 3.1%.
Amezitaka kila halmashauri kuhakikisha zinatenga fedha zinazotokana na 10% ya mapato ya ndani ili kutoa mikopo kwa wanawake 4%, vijana 4%, na walemavu 2%, ambapo katika mwaka wa fedha 2022/2023 Mkoa wa Ruvuma jumla ya fedha Mil.58,825,492.4 zilitolewa kwa vikundi 93 ikiwa ni sehemu ya fedha zilizotolewa za 10% ya mapato ya ndani ya halmashau
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Komredi Oddo Mwisho amewataka viongozi, wanawake na Asasi mbalimbali kukemea na kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ambao unaendelea kufanywa ili kuondoa mila na desturi potofu zinazowakandamiza wanawake na kuongeza ufahamu juu ya haki na usawa katika jamii.
KAULI MBIU; ubunifu na mabadiliko ya Teknolojia ni chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa