NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA,
03.09.2021.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ameongoza kikao cha uzinduzi wa bodi ya huduma ya Afya Halmashauri ya Manispaa ya Songea, kikao kilichofanyika leo tarehe 3 Septemba 2021 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Katika kikao hicho Mgema amesema kuwa mwaka 1994 Wizara ya afya ilianza utekelezaji wa maboresho katika Sekta ya afya na Sekta nyingine ili jamii iweze kuwa na madaraka zaidi ya kuamua kuhusu huduma za afya zinazotolewa pamoja na kushiriki kikamilifu katika utoaji wa huduma hizo kwa kuunda Bodi za Huduma za Afya za Halmashauri na Kamati za vituo vya huduma.
Aliongeza kuwa bodi hiyo ina jukumu kubwa la kuendelea kuihamasisha jamii kujiunga na mfuko afya ya jamii iCHF iliyoboreshwa ambayo sio tu ni chanzo cha mapato bali pia ni mkombozi wa wananchi kupata huduma ya afya kwa gharama nafuu ambapo lengo la taifa ni kufikia asilimia 30% ya usajili wa kaya katika mfuko huo wa afya ya jamii “Mgema alieleza”.
Mgema alibainisha kuwa Serikali imetoa fedha za kujenga miundombinu ya kutolea huduma za afya pamoja na kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya afya ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Songea imepata vituo vingi zaidi vya afya kuliko Halmashauri nyingine zote pamoja na fedha za ukamilishaji wa zahanati kubwa 4 ambazo zinaombewa usajili ili ziwe vituo vya afya.
Bodi ya huduma ya afya imeweka mikakati ya upatikanaji wa miundombinu ya kutosha kwa kufanya ukarabati wa majengo yaliyopo na ujenzi wa majengo mapya pamoja na kuboresho mawasiliano na mfumo wa taarifa.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa