Na;
Amina pilly;
Mkuu wa wilaya ya songea , Mhe. Polelet Kamando Mgema amewataka wenyeviti pamoja na watendaji kata/mitaa wa manispaa ya songea kutoa ushirikiano katika zoezi la sensa itakayofanyika tarehe 23 agosti 2022.
Rai hiyo imetolewa tarehe 20 agosti 2022 katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa manispaa ya songea kwa lengo la kuwahimiza viongozi hao kushirikiana kikamilifu pamoja na makarani wa sensa ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi kwa dhumuni la kupata takwimu sahihi zitakazo saidia kupanga miradi mbalimbali ya maendeleo
Polelet alitoa maagizo ya kuwa kila kiongozi anatakiwa kuwajibika kwa kupeleka ujumbe kwa wananchi kupitia agizo la Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa “ siku ya jumanne itakuwa siku ya mapumziko kwa watumishi wote wa serikali,” ili wananchi wote waweze kujitokeza kikamilifu na kufanikisha zoezi hilo.
Aliongeza kuwa wenyeviti na watendaji wote kufikisha taarifa kwa wananchi wote ambao wanamiliki mashamba katika maeneo yaliyopo nje ya manispaa ya songea kujitokeza kusajiliwa katika maeneo hayo ili waweze kupata pembejeo za kilimo kwa urahisi zaidi.
MWISHO.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa