Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro (MB) amewataka wananchi kuunga mkono jitihada za Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani ili kuleta msukumo wa maendeleo katika Taifa letu.
Hayo yamejiri katika ziara ya iliyofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 18 Julai 2023 ambapo ametembelea kata Ruvuma, Kata ya Tanga, kata Lilambo, Kata ya Mshangano, Kata ya Msamala, pamoja na kata ya Bombambili kwa lengo kukagua hatua mbalimbali za miradi ya maendeleo.
Dkt. Ndumbaro amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuchangia nguvu kazi katika Shughuli mbalimbali zinazoendelea katika kata na mitaa.
Alisema tarehe 22 Julai 2023 kutakuwa na ugeni wa ujio wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ambaye atazungumza na wananchi katika uwanja wa Majimaji kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa