Mstahiki Meya Manispaa ya Songea amewataka wananchi kushiriki uchaguzi Mkuu na kuchagua viogozi bora watakaoleta maendeleo katika jamii.
Kauli hiyo imetolewa kwenye mkutano wa hadhara wa kusoma ilani ya utekelezaji wa chama cha mapinduzi kata ya Lilambo iliyosmwa na Diwani Yobo Mapunda katika kipindi cha miaka 5.
Kata ya lilambo ni miongoni mwa kata 21 ambayo ina diwani mmoja wakuchaguliwa na diwani wa viti maalumu ambapo kupitia chama chake cha CCM Diwani Yobbo Mapunda amesoma Ilani ya utekelezaji katika kipindi cha miaka 5 kuanzia 2020 hadi 2025.
Akisoma Ilani hiyo mbele ya wananchi wa kata hiyo chini ya viongozi wake wa CCM Wilaya ya Songea Mjini, viongozi ngazi ya kata na matawi alisema katika kipindi cha miaka mitano kata ya Lilambo imejenga Zahanati 4 na Kituo cha afya 1 kimoja kilichojengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.
SKTA YA ELIMU:
Kata ya Lilambo ina jumla ya Shule 8kwa mchanganuo ; · Shule za Sekondari 2 zenye mchanganyiko wavulana na wasichana · Shule za Msingi 6 · Shule Shikizi 1 · Idadi ya wanafunzi 3132, kati ya hao, Wavulana 1511 na Wasichana 1621. · Idadi ya walimu 115 kati ya hao Wanaume 63 na wanawake 52.
Aidha, Kata ya Lilambo imefanikiwa kupokea jumla ya Tshs 535,600,000/= ambapo 529,400,000/ ni jumla ya mapato kutoka serikali kuu, Halmashauri ya Manispaa Songea pamoja na mfuko wa jimbo na Tshs 6,400,000/= nguvu za wananchi ambapo fedha hizo zimetekeleza miradi Tshs 84,000,0000/= ujenzi na ukamilishaji wa jengo la hostel ya chabruma sekodanri, kati ya hizo tshs 4,000,000/= ni nguvu za wananchi jengo linatumika.
Aliongeza kuwa Tshs 52,000,000/= ujenzi na ukamilishaji wa maabara katika shule ya sekondari ya chabruma kazi imekamilika, Tshs 40,000,000/= ujenzi wa madarasa 2, viti 100 na meza 100 Sekondari ya Chabruma kazi imekamilika, Tshs 60,000,000/= ujenzi wa madarasa 3, viti 150, meza 150 sekondari ya Sili kazi imekamilika.
Sambamba na hilo Tshs 30,000,000/= ujenzi wa maabara Sili sekodanri kazi imekamilika 6. Ths 26,200,000/= ujenzi wa madarasa 2 , ofisi 1 shule ya msingi Luwawasi kati ya hizo nguvu za wananchi ni 1,200,000/= 7. Tshs 11,200,000 ujenzi wa matundu 10 shule ya msingi Likuyufusi kati ya hizi nguvu za wananchi ni 1,200,000/= kazi inaendelea 8. Ths 5,000,000/= ukamilishaji madarasa 2 na ofisi 1 shule shikizi Lilambo "B" 9. Tshs 5,000,000/= ujenzi wa matundu 4 ya vyoo shule ya msingi mang'ua kazi inaendelea, pia Tsh.192,000,000/ ujenzi wa madarasa 8 pamoja na viti 50 na meza 50 kwa kila darasa hayo Shule ya Sekondari SILI. ujenzi umekamilika ambapo Tsh.10,000,000/ utengenezaji wa madawati 153 kwa shule za msingi. Kwa mgawanyo ufuatao: sinai 25, Likuyufusi 55, Mangua 35, Lilambo38.
Miradi mingine ni Tsh.25,200,000/ Ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Chabruma. Ujenzi unaendelea. 13. Tsh.7,200,000/ Ukamilishawa ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja shule shikizi Lilambo B, mradi bado haujaanza mzabuni bado hajapatikana, Tsh.8,000,000/ Manunuzi ya vitanda 40 katika shule ya Chabruma Sekondari, fedha kutoka mfuko wa Jimbo ofisi ya Mh.Mbunge Songea Mjini. 2 Mifumo ya gesi kwenye Jengo la Maabara vyumba vyote viwili katika shule ya sekondari Sili na sehemu ya nje ya jengo maabara zinatumika Luwawasi vimekamilia na vinatumika.
Alifafanua kuwa Jengo la Maabara mbili katika shule ya Sekondari Sili likiwa limekamilia na tayari maabara zinatumika. vimekamilia na vinatumika. 3 Vyumba viwili vya Madarasa pamoja na ofisi katika shule ya msingi Luwawasi vimekamilia na vinatumika. Vyumba vitatu vya Madarasa katika shule ya Sekondari ya Sili vimekamilia na vinatumika. 4 5 Hostel ya wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari ya Chabruma imekamilika na inatumika. Vitanda katika vyumba vya Hostel ya wanafunzi wa kike shule ya Sekondari ya Chabruma ikiwa katika matumizi ya wanafunzi wa kike. Muonekano wa ndani katika Hostel ya wanafunzi wa kike shule ya Sekondari ya Chabruma. Tanki la kuhifadhia maji kutoka kwenye kisima kirefu kinachotumia pampu ya umeme –Shule ya sekondari Chabruma . Jumla Vyumba nane (8) vya Madarasa, viti na Madawati 50 kwa kila darasa vikiwa vimekamilika na kuanza kutumika . 6 Mradi wa Ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Chabruma Chabruma na Ujenzi unaendelea na kuanza kutumika .
Mhe Yobo akikabidhi madawati 153 kwa shule za msingi za Sinai,Likuyufusi, Mangua na Lilambo38 Baadhi ya majengo katika shule Shikizi Lilambo B 7 4. SEKTA YA AFYA ambapo Katika Sekta ya afya Kata ya Lilambo in jumla ya zahanati 5 kati ya hizo moja iko chini ya jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) kambi ya Chabruma , Kwa kipindi hicho Kata ya Lilambo imefanikiwa kutekeleza miradi miwili (2) iliyogharimu jumla ya Tshs 524,295,000/= kwa mchanganuo ufuatao :- (l) Jumla ya Tsh.517,295,000/= zimetekeleza mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Lilambo, kati ya fedha hizo, Tshs.514,000,000/, kutoka Kwa Mkurugenzi Manispaa ya Songea, ni fedha zilizotokana na Mapato ya Ndani ya Halmashauri, na Tshs. 3,295,0001 ikiwa ni nguvu za Wananchi.
MIKOPO 10%
Kata ya Lilambo kwa kupitia Mpango kazi wa Halmashauri yetu Kata hii ina eneo la viwanda. majengo ya viwanda vifuatavyo yameshajengwa na kukamilika kwa kupitia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashari nayo ni Jengo la ushonaji, linafanya kazi. Jengo la kukamua mafuta ya Alizeti, linafanya kazi. Jengo la kutengeneza batiki, linafanya kazi. Jengo la Uchomeleaji vyuma na Alminiamu, linafanya kazi. Jengo la Kusindika Asali, bado halijaanza kufanya kazi, Jengo la Uselemala linafanya kazi, Jengo la kutengeneza vifungashio linafanya kazi Jengo la Ofisi ya wamachinga ambapo kati ya majengo hayo jengo la kukamua mafuta ya Alizeti ni kikundi cha wanawake wa kutoka katika Kata hii ya Lilambo.
Aidha, eneo hilo la viwanda kuna miradi inayotarajiwa kujengwa kama ujenzi wa barabara km.l na nusu kwa kiwango cha lami,ujenzi wa ghala la kuchakata 10 mazao, ujenzi wa kituo cha polisi , ni miradi itakayotekelezwa kwa fedha za Benki ya Dunia.
Pia vipo vikundi ambavyo vimekopeshwa fedha katha vile kikundi cha Pambazuko Sinai wanajishuhuguilisha na kilimo, kikundi cha Agape wanawake Lilambo 'B' wanashughulika na ufugaji wa Nguruwe, kikundi cha MOMI walemavu toka Likuyufusi wamekopeshwa fedha na wamenunua bajaji inafanya kazi. Hizo ni fedha kutoka 10 % ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Sekta ya Biashara, Kata imepokea Jumla ya Tshs.460,000,000/ kwaajili ya ujenzi wa pakingi ya magari makubwa Maroli, ni mradi ambao unatekelezwa katika Mtaa wa Lilambo A. Mradi huu umetengewa bajeti ya Tsh.1,027,654,254.71/ (bilioni moja na milioni ishirini na saba na miasita na hamsini na nne na miambili hamsini na nne na senti sabini na moja tu)' ambapo Mradi huo unatekelezwa na mkandarasi aitwaye EIMA GENERAL SUPPLIES CO.LIMITED, ni mradi ambao umeanzwa kutekelezwa tarehe 1 march 2025 na utakamilika tarehe 1 September 2025
SEKTA YA MAJI:
Katika mradi wa maji SOUWASA ilitekeleza mradi wa kusambaza maji kwa Tshs. 930,000,000/= mtaa wa Lilambo A na B hadi eneo la viwanda na kwa wananchi wa jirani wa maeneo ya viwanda kuna mradi wa maji uliotekelezwa wa Tshs. 400,000,000/= Mtaa wa Sinai - Ujenzi wa mradi wa maji ya mtirirko 13 Mh.mwenyekiti pia kuna mradi wa maji tiririka mtaa wa sinai na Mang'ua wenye kughalimu Tsh.1,500,000,000/ mradi unaotekelezwa na SOUWASA fedha kutoka serikali kuu. Sehemu ya Mabomba yaleyopokelewa tayari kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa Maji utakaotekelezwa na SOUWASA katika Mitaa ya Sinai, Lilambo A na Lilambo B 9.
Kata ya lilambo pia imepokea mchango kutoka kwa Mh. Mbunge na Mstahiki kiasi cha shilingi 3,500,000 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa katoliki luwawasi Mhe. Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dr. Damasi Ndumbaro , Mstahiki Meya, Diwani wa Kata ya Lilambo na Viongozi wengine akikabidhi Mchango kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jumla ya Tsh 3,5000,000.
SHUKRANI
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Wananchi wa Kata hii ya Lilambo, Napenda kutoa Shukrani kwa Mh. Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha na miongozo mizuri ya usimimizi na utekelezaji wa shughuli za maendeleo, na yenye kuleta matunda mazuri. Pia tunatoa shukrani kwa Mh.Mbunge wetu wa Jimbo la Songea mjini, Dkt. Damas Ndumbaro, Mhe. Mstahiki Meya na baraza lake, Mhe. Yobo Xavery Mapunda, Diwani wa Kata hii, pamoja na Wenyeviti wa serikali za mitaa na Wataalamu wote ngazi ya kata na Watendaji wamitaa kwa usimamizi wenu mzuri katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha 2020 - 2025.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa