Katibu Mkuu CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amefanya ziara ya kutembelea Halmashauri nne zilizoko Mkoani kwa lengo la kupokea kero mbalimbali kutoka wananchi na kuhamasisha wanchama kujisajili.
Akizungumza na wananchi katika uwanja wa Matarawe Manispaa ya Songea alisema “ Serikali ya awamu ya sita inaendelea kutoa pembejeo za ruzuku kwa wakulima ambapo imewezesha kuongezeka kwa mazao kwa wakulima ambayo kwa muda wa miaka mitano 5 Mfululizo Mkoa wa Ruvuma unaongoza kwa mavuno mengi ya chakula”
Alisema katika kuboresha mikopo ya vikundi inayotelewa ya 10% kwa wanawake 4%, Vijana 4% na walemavu 2%, Serikali imetenga bajeti ya Bil 229 kwa nchi nzima kati ya hiyo Mkoa wa Ruvuma umetengewa kiasi cha Bil. 2.2 ambayo itatolewa kuanzia julai 2024. “ alibainisha.”
Ziara hiyo imefanyika Manispaa ya Songea terehe 20 Aprili 2024 ambayo itahitimishwa tarehe 22 aprili 2024 katika Halmshauri ya Wilaya ya Songea.
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa