Kamati ya fedha na uongozi Manispaa ya Songea ikiongozwa na Naibu Meya Manispaa ya Songea Mheshimiwa Jeremiah Mlembe, imefanya ziara ya kutembelea na kukagua vyanzo mbalimbali vya mapato vya Halmashauri iliyofanyika leo tarehe 28 Februari 2024.
Miongoni mwa vyanzo vya mapato vilivyotembelewa ni pamoja na Vibanda na vyoo vya Stendi kuu ya mabasi Songea, Soko la mazao Msamala, vibanda na Vyoo vya Mfaranyaki na Majengo, Machimbo ya Madini ya ujenzi Lilambo, Standi ya Seedfarm, na Stand ya Ruhuwiko.
Jeremiah alisema “ Lengo la ziara hiyo ni kufanya ufuatiliaji, na kukagua utekelezaji wa vyanzo vya mapato na kubaini changamoto mbalimbali za ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa