Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uwekezaji Mkoa wa Ruvuma Jeremiah Sendoro amewataka wataalamu Manispaa ya Songea kuhakikisha wanendelea kufuatilia na kusimamia kwa weredi miradi yote inayoendelea kujengwa ili iweze kukamilika kwa wakati.
Miongongoni mwa miradi iliyotembelewa na timu ya wataalamu kutoka ofisi RS Ruvuma ni pamoja na ujenzi wa madarasa 7 Sekondari ya Mdandamo inayojengwa kwa gharama ya Mil. 170.5, ukamilishaji wa Hospitali ya Manispaa ya Songea (jengo la utawala,stoo ya dawa na Wodi ya wazazi ) inayojengwa kwa gharama ya mil. 800 fedha kutoka Serikali kuu.
Miradi mingine iliyotembelewa ni ujenzi wa madarasa 4 na matundu 10 ya vyoo Sekondari ya Msamala inayojengwa kwa Mil. 115.5, ukamilishaji wa matundu ya vyoo Shule ya Msingi Shikizi Mkuzo inayojengwa kwa Mil. 10 fedha za mapato ya ndani, Ujenzi wa madarasa 8 shule ya Sekondari Siri inayojengwa kwa Mil. 192 fedha kutoka Serikali kuu, pamoja na ujenzi wa madarasa 10 shule ya Sekondari Londoni inayojengwa kwa Mil. 242.5 fedha kutoka Serikali kuu ambao upo hatua ya ukuta.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 23 Februari 2024 ambayo ilishirikisha wataalamu kutoka ofisi ya Mkoa wa Ruvuma pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa