SHUGHULI muhimu za kiuchumi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ni Kilimo na biashara ambapo Kilimo huchangia asilimia 75 ya pato la Halmashauri. Mazao yanayowapatia wananchi Mapato makubwa ni Mahindi na Mpunga, aidha pato la mkazi wa Manispaa ya Songea ni Tshs, 738,022.00 kwa mujibu wa ripoti ya GDP iliotolewa na ofisi ya Taifa ya Takwimu mwaka 2006. Kwa sasa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ipo katika hatua za mwisho za kukokotoa pato la mkazi kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili kujua pato la mkazi kwa sasa.
Kwa sasa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ipo katika hatua za mwisho za kukokotoa pato la mkazi kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili kujua pato la mkazi kwa mwaka.
Dira ya Halmashauri ni kuwa kitovu cha uwekezaji na maendeleo ya viwanda ili kufikia maendeleo endelevu ya jamii 2025.
Kwa sasa Halmashauri inakadiriwa kuwa na idadi ya Watu 252,150 wakiwemo Wanaume 119,182 na Wanawake 132,968 kutokana na ongezeko la asilimia 4.4 kwa mwaka, Aidha ina jumla ya Kaya 61,930 kwa wastani wa watu 4.2 kwenye kila kaya.
Halmashauri ina jumla ya Mitaa 95, Kata 21 na Tarafa 2. Halmashauri ina jumla ya waheshimiwa madiwani 28, kati yao 21 ni wa kuchaguliwa, 7 ni wawakilishi Viti Maalum. Halmashauri inalo jimbo moja la uchaguzi ambalo Mbunge wake ni Mhe. Damas Ndumbaro na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Jackline Ngonyani.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa