ZIWA Nyasa linapita katika wilaya za Nyasa mkoani Ruvuma,wilaya ya Ludewa mkoani Njombe na wilaya ya Kyela mkoani Mbeya’
Utafiti umebaini kuwa Ziwa Nyasa lina aina zaidi ya 400 za samaki wa mapambo ambao hawapatikani katika maziwa, mito na bahari sehemu nyingine yeyote katika sayari ya Dunia.
Tafiti zinaonesha kuwa katika Sayari inayoitwa Dunia,hakuna ziwa lenye samaki wa mapambo aina zaidi ya 400,ni ziwa Nyasa pekee,ambalo pia linaongoza duniani kwa kuwa na viumbe wengi katika maziwa yenye maji baridi pia ziwa hilo linaongoza kwa kuwa na maji maangavu.
Kulingana na utafiti ambao ulifanywa na Jumuiya ya nchi zilizo Kusini mwa Afrika(SADC) kwa kushirikiana na nchi ya Uingereza kwenye ziwa Nyasa kati ya mwaka 1991 hadi 1994 na mwaka 1996 hadi 2000,ulionesha kuwa ziwa hilo lina kiasi cha tani 165,000 za samaki na kati ya kiasi hicho tani 35,000 za samaki.Ziwa Nyasa lina aina 1500 za samaki.
Ziwa Nyasa limezungukwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania,Malawi na MsumbIji.Ziwa hilo lipo kwenye usawa wa meta 500 toka usawa wa bahari ambapo kina cha ziwa hilo ni karibu meta 750,urefu wake ni karibu kilometa 1000 , upana mkubwa ni kilometa 80 na upana mdogo ni kilometa 15.
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa nchini ambayo imejaliwa kuwa na maeneo ya hifadhi na vivutio vizuri vya utalii kama vile Makumbusho ya Taifa ya Majimaji, Mapango ya Chandamali,majengo ya kihistoria Peramiho, samaki wa mapambo, fukwe na visiwa katika ziwa Nyasa.
Vivutio vingine ni maeneo ya wapigania uhuru nchi za kusini mwa Afrika,mapori ya wanyamapori ya Liparamba, Selous, Litumbandyosi na misitu ya asili ukiwemo msitu katika milima ya Matogoro ambao ni chanzo cha Mto Ruvuma unaomwaga maji yake Bahari ya Hindi.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Mei 14,2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa