MTAZAME Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha alipotembelea Sekondari ya Songea Girls ambayo inakarabatiwa na Wakala wa Majengo Tanzania(TBA).Waziri amesikitishwa na TBA kuwa nyuma ya mkataba kwa mwaka mmoja hali ambayo inaleta changamoto kubwa kwa wanafunzi zaidi ya 800 wanaosoma katika sekondari hiyo.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknlojia William Ole Nasha amekutana na walimu wa shule ya sekondari ya Songea Girls na kutoa ufafanuzi kuhusu Bodi ya Taaluma ya Walimu wa Tanzania
Naibu Waziri Elimu,Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kuhakikisha wanaanzisha kozi ya ufundi wa zana za kilimo (agro mechanics) na kozi ya utalii katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Songea VETA ili kuweza kupata vijana wengi watakaoweza kusoma kozi hizo.Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa chuo hicho toka kwa Mkuu wa Chuo cha VETA Songea Gideon Ole Laurumbe akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili katika wilaya za Songea na Namtumbo.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa