September 27, 2018 ni siku ya 8, tangu kuzama kwa meli ya Mv. Nyerere na hadi leo ni siku 4, tangu zoezi la kukinasua Kivuko kutoka ndani ya maji lianze linaongozwa na Mkuu wa Majeshi Venance Mabeyo.
Luteni Kanali Mstaafu Daniel Gangisa (90) ni mmoja wa Brigedi Kamanda aliyeongoza vikosi kumng,oa Dikteta Idd Amini Dada katika ardhi ya Tanzania hadi Uganda mwaka 1979.Shujaa wa Tanzania,Gangisa ni Mstaafu wa JWTZ ambaye anaishi katika Kitongoji cha Chandarua Kata ya Mshangano Wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma.
Gangisa alisoma na Idd Amini nchini Kenya kuanzia mwaka 1953,1954 hadi mwaka 1955 ,waliishi bweni moja ,chumba kimoja na kulala kitanda cha double decker mmoja chini na mwingine juu.walikutana tena na Idd Amini mwaka 1960 Nakuru nchini Kenya.
AFISA Utumishi Mkuu wa Manispaa ya Songea mkoani RUVUMA Lewis Mnyambwa amewatahadharisha watumishi wapya kuwa makini na mikopo inayotolewa na baadhi ya Taasisi za fedha badala yake amewashauri kukopa katika Taasisi za serikali kama Benki ya NMB ambayo mishahara ya watumishi wengi inapitia huko. Mnyambwa alikuwa anazungumza katika Kikao kazi cha watumishi wapya zaidi ya 100 ambao wameajiriwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017.Katika kikao hicho mada mbalimbali zimefundishwa zikiwemo kanuni za maadili ya utendaji katika Utumishi wa umma,HAKI,wajibu na stahili za watumishi wa umma,mfumo wa upimaji wa utendaji kazi katika Utumishi wa umma na mwongozo wa mavazi katika Utumishi wa umma.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa