NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege amekagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea .Moja ya miradi ambayo ameikagua na kutoa maelekezo ni mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ruvuma ambao unagharimu shilingi milioni 400 katika awamu ya ujenzi.Mradi huo ni wa miezi sita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Agosti, 2018 amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya 1, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 41, na amewahamisha vituo vya kazi Mkuu wa Wilaya 1 na Wakurugenzi wa Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 19.
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege yupo mkoani Ruvuma katika ziara kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo,akiwa katika Manispaa ya Songea ameikagua barabara ya Tumbani eneo la majengo Kandege amemwagiza Mkandarasi kuhakikisha kuwa barabara hiyo inawekwa lami nzito kabla ya mvua za masika hazijaanza Novemba mwaka huu kwa kuwa mvua zikiianza inakuwa ni kazi ngumu kuweka lami hivyo amewaagiza kuongeza kasi ili kusiwepo na kisingizio cha mvua.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa