CHUO pekee kinachotoa mafunzo ya Ufamasia katika ukanda wa Kusini kimeanzishwa katika Kata ya Msamala Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Mkurugenzi wa Kampuni ya TOPONE LIMITED ambao ndiyo wamiliki wa Chuo hicho Pascal Msigwa amesema chuo hicho kinatarajia kufunguliwa Oktoba mwaka huu ambacho kwa kuanzia kitakuwa kinatoa mafunzo ngazi ya cheti ambayo yanachukua miaka miwili.Msigwa amesema chuo hicho kimesajiriwa na Baraza la Ufundi la Taifa (NACTE) na kupewa namba ya usajiri 184 na kwamba lengo la kuanzisha chuo hicho kuiunga mkono serikali ya
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameridhishwa na wimbo uliotungwa na kuimbwa na kwaya ya JKT Mlale wilayani Songea mkoani Ruvuma wa kuhamasisha kampeni ya Furaha Yangu na kuagiza sasa wimbo huo utakuwa wa kitaifa katika kuhamasisha kampeni hizo ambazo zinafanyika nchini nzima.Waziri Mwalimu akiwa na meza kuu akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme walilazimika kusimama na kwenda kuungana na kwaya hiyo katika uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu mkoani Ruvuma ndani ya uwanja wa Majimaji mjini Songea.Waziri huyo wa afya amesema serikali itasimamia kuhakikisha wimbo huo unarekodiwa na kutumika rasmi kitaifa katika kampeni hizo ambazo zinazinduliwa ngazi ya mikoa na kuendelea hadi katika ngazi ya wilaya.
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema serikali kuanzia mwaka 2019 inatarahis kutoa dawa Mpya ya kufubaza virusi vya UKIMWI.Mwalimu amesema hayo wakati anazindua kampeni ya Furaha Yangu ngazi ya mkoa wa Ruvuma ndani ya uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa