NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Sinkamba Kandege yupo mkoani Ruvuma ambapo anatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.Naibu Waziri huyo wa TAMISEMI amekagua mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa katika Kata ya Tanga manispaa ya Songea.Mradi huo ambao umefikia Zaidi ya asilimia 60 unatarajia kukamilika Oktoba mwaka huu ambapo hadi sasa Mkandarasi ameshalipwa Zaidi milioni 900 ambayo ni asilimia 35 ya malipo ya mradi huo ambao unagharimu Zaidi ya bilioni 3.2.
MRADI wa machinjio ya kisasa ya Songea umefikia Zaidi ya asilimia 60 unatarajia kukamilika Oktoba mwaka huu ambapo hadi sasa Mkandarasi ameshalipwa Zaidi milioni 900 ambayo ni asilimia 35 ya malipo ya mradi huo ambao unagharimu Zaidi ya bilioni 3.2.Akitoa taarifa ya mradi huo,Kaimu Mhandisi wa Ujenzi wa Manispaa ya Songea Mhandisi Nicolus Danda amesema mradi wa machinjio ya kisasa unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya shilingi bilioni 3.2.
MTAZAME Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaj Abdul Hassan Mshaweji akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa TAMISEMI Josephat Kandege alipotembelea na kukagua stendi ya kisasa ya mabasi ya Songea ambayo inajengwa katika Kata ya Tanga kilometa 14 toka mjini Songea.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa