MTAZAME Mkuu mpya wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akizungumzia programu maalum ambayo anatarajia kuanzisha katika wilaya hiyo ili kupunguza changamoto ya mimba za utotoni katika wilaya yake
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametoa maagizo mazito ya kuhakikisha Halmashauri zote zinakusanya mapato kwa asilimia 100 na kwamba Halmashauri ambayo itashindwa kufikia malengo atashauri ifutwe au kushushwa daraja.Mndeme alikuwa anazungumza na watendaji wa Halmashauri zote za mkoa wa Ruvuma mara baada ya kumuapisha Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo katika sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma mjini Songea.Sherehe hizo zimehudhuria na viongozi mbalimbali katika ngazi za wilaya na mkoa .
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amemwapisha mkuu wa wilaya Mpya wa Namtumbo Sophia Kizigo ili aweze kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia wananchi wa Namtumbo.Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa mkoa na kuhudhuriwa na watendaji mbalimbali ngazi za wilaya na mkoa
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa