HIFADHI ya Taifa ya wanayama pori ya Serengeti nchini Tanzania imeibuka ya kwanza Afrika baada ya utafiti uliofanywa na kampuni ya utalii ya Safari Bookings, utafiti uliofanyika mtandaoni kupitia tovuti yake.
Hifadhi hiyo imepata alama 4.9 kati ya 5. Mwaka 2015 Serengeti ilishinda na kuwa hifadhi bora zaidi.Moja ya sababu za hifadhi hiyo kuwa bora zaidi ni uwepo wa wanyama wengi wakiwemo aina tano kubwa (Big Five) ambao ni Tembo, Simba, Faru, Chui na Nyati.Sababu nyingine ni kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni limetaja eneo hilo kuwa urithi wa dunia.
MWENYEZI Mungu kila kiumbe amempa uwezo wa kupambana na maadui hata kuweza kujipatia ridhiki yake.Hebu tazama maajabu ya kiumbe hiki kidogo sana ambacho unaweza kukiua kwa vidole kilivyofanikiwa kumwangamiza nyoka na kujipatia kitoweo
Mradi wa ULGSP, ambao unasimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ,unatekelezwa katika Halmashauri ya Manispa ya Songea ikiwa ni miongoni mwa Halmashauri 18 nchini zinazotekeleza mradi huo.Tazama Master Plan ya Mji wa Songea ambao utaifanya Songea mpya yenye muonekano wa kuvutia kwa kila mmoja ambaye atabahatika kutembelea Songea ambayo ndiyo makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa