Mjusi huyo alivumbuliwa katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi miaka 100 iliyopita.Mjusi huyo ni kuvutio adimu katika makumbusho ya Berlin nchini Ujerumani ambaye ana uzito wa tani 50.Mjusi huyo anakadiriwa kuwa na umri wa miaka milioni 150,ana urefu wa meta 13.7 kwenda juu,anakadiriwa kuwa na moyo wenye uzito wa kilo 400 na chakula cha mjusi huyo kilikuwa ni mimea.mjusi huyo aligundulika kati ya mwaka 1907 na 1909
Makumbusho ya Taifa ya Majimaji yaliyopo Manispaa ya Songea, yamehifadhi vifaa na silaha halisi ambazo walitumia mashujaa hao kupambana na wakoloni wa kijerumani
Hii ni Makumbusho pekee nchini ambayo imebahatika kuwa na vifaa vyote asilia na muhimu katika historia ya mtanzania hali ambayo inaitofautisha makumbusho nyingine tanoTaifa za zilizopo hapa nchini.
SIku ya sokwe duniani imetangazwa na umoja wa mataifa kuwa itakuwa inaadhimishwa kila mwaka Julai 14.Tunapoelekea katika maadhimisho hayo tuangalie maisha ya sokwe.Sokwemtu anabeba mimba kwa muda wa miezi nane na nusu.lakini pia ananyonyesha kwa muda wa miezi sita,binadamu wanachagua marais,lakini pia sokwe wanachagua marais wao ambao wanapatikana kwa kupigana ambapo sokwe anayeshinda ndiyo anakuwa kiongozi wa sokwe.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa