MTAZAME Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Tina Sekambo akizungumzia maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika Manispaa ya Songea ikiwemo inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ambayo ni ujenzi wa barabara za lami,ujenzi wa machinjio ya kisasa,ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa na ujenzi wa bustani ya manispaa ya Songea.Pia Manispaa inatekeleza miradi mingine mingi ya maendeleo.
SHULE ya sekondari ya wavulana Songea (Songea Boys) iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imewekwa katika mpango wa kuletewa kiasi cha shilingi milioni 325 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matano na mabweni matatu.Timu ya wataalam wa Manispaa ya Songea ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo imetembelea shule ya sekondari ya wavulana Songea, eneo ambalo litajengwa madarasa matano na mabweni matatu.
MTAZAME Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamis Kigwangalla akizungumzia kivutio cha utalii cha Maporomoko ya Kimani kilichopo kusini.Kigwangallah anaelezea umuhimu wa eneo hilo kama moja na vyanzo vya maji vinavyotegemewa hapa nchini
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa