MKUU wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,Pololet Mgema amezindua rasmi Bodi ya Huduma za Afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Akizungumza kabla ya uzinduzi wa Bodi hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema ameiagiza Bodi hiyo kusimamia dawa za serikali kuhakikisha dawa hizo zinalindwa kwa kuwa ni rasilimali za umma hivyo zinatakiwa kutumika kwa ajili ya wananchi wote.
Mzee mmoja wa umri wa miaka 60 amewashangaza wanakijiji wa Mugono Kiharu nchini Kenya kwa kubadilisha kitanda chake kuwa nyumba anamoishi katikati ya shamba lake dogo kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni kufilisika kwa hali ya juu. Kamau Mwangi amekuwa akiishi katika hali hiyo kwa miaka 6 sasa baada ya kuuza shamba lake la ekari mmoja lenye thamani ya zaidi ya milioni nane kwa fedha za Tanzania na fedha yote kumaliza kwa ulevi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Aloyce Nzuki akielezea namna serikali ilivyodhamiria kurejesha fuvu la kichwa cha shujaa Songea Mbano toka nchini Ujerumani ambako kimehifadhiwa tangu mwaka 1906.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa