Mzee mmoja wa umri wa miaka 60 amewashangaza wanakijiji wa Mugono Kiharu nchini Kenya kwa kubadilisha kitanda chake kuwa nyumba anamoishi katikati ya shamba lake dogo kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni kufilisika kwa hali ya juu. Kamau Mwangi amekuwa akiishi katika hali hiyo kwa miaka 6 sasa baada ya kuuza shamba lake la ekari mmoja lenye thamani ya zaidi ya milioni nane kwa fedha za Tanzania na fedha yote kumaliza kwa ulevi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Aloyce Nzuki akielezea namna serikali ilivyodhamiria kurejesha fuvu la kichwa cha shujaa Songea Mbano toka nchini Ujerumani ambako kimehifadhiwa tangu mwaka 1906.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii Meja Generali Gaudance Milanzi amesema wanaojihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo, ni vema kuacha biashara hiyo kwa kuwa mtandao uliowekwa na serikali dhidi ya majangili umesababisha biashara ya meno ya tembo kukosa soko na wahusika wote kukamatwa na vyombo vya dola. Katibu Mkuu huyo ànawashauri majangili sasa kufanya kazi nyingine halali ili wasiingie kwenye mkono wa sheria.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa