HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea kupitia program ya maji na usafi wa mazingira inaendelea kukarabati visima vya maji 89 lengo ni kuongeza utoaji huduma ya maji kwa wananchi.Mradi huo unaotekelezwa katika kata 10 unagharimu zaidi ya shilingi milioni 294.Hadi sasa visima 61 vimekarabatiwa bado visima 28.
KAMATI ya Fedha na Uongozi ya Baraza la Madiwani katika Manispaa ya Songea imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mradi huu wa ukamilishaji wa choo na zahanati ya Bombambili.
KAMATI ya Fedha na Uongozi ya Baraza la Madiwani la Manispaa ya Songea, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Goden Sanga imekagua mradi wa machinjio ya kisasa unaotekelezwa katika Kata ya Tanga Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Akitoa taarifa ya mradi huo kwa Kamati hiyo kabla ya kuanza ukaguzi,Kaimu Mhandisi wa Ujenzi wa Manispaa ya Songea Mhandisi Nicolus Danda amesema mradi wa machinjio ya kisasa unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya Zaidi ya shilingi bilioni 3.2.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa