MKOA wa Ruvuma sasa utakuwa na migodi miwili, ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe ukiwemo mgodi wa Ngaka wilayani Mbinga na sasa KAMBAS Muhukuru Songea.MGODI upo umbali za zaidi ya kilometa 150 toka mjini Songea.Lengo la Mgodi ni kuzalisha kati ya tani 600 hadi 700 kwa siku ambapo kwa mwezi Mgodi utakuwa na uwezo wa kuzalisha makaa ya mawe kati ya tani 18,000 hadi 21,000 kwa mwezi.Hadi sasa Mgodi wa KAMBAS umetoa ajira rasmi 20 na ajira ambazo sio rasmi 50
MRADI wa ujenzi wa stendi ya kisasa ya Tanga Manispaa ya Songea ambao umeanza Mchi 25,2018 na unatarajia kukamilika Septemba 30,2018.Mradi huu katika awamu ya kwanza unagharimu zaidi ya bilioni sita ambapo tayari mradi umefikiaasilimia 30.
Kwa mujibu wa Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Songea Karoline Bernad,kazi ambazo zinafanyika awamu ya kwanza katika stendi hiyo ni ujenzi wa lami nzito yenye kilometa mbili,taa barabarani,maduka 30,vibanda 20 vya tiketi,jengo la utawala,vyoo vya matundu 12 na eneo la kupaki magari.Mradi huo unafadhiliwa naBenki ya Dunia ambapo hadi sasa Mkandarasi amelipwa zaidi ya shilingi bilioni 444.
TAZAMA mradi wa machinjio ya kisasa katika Kata ya Tanga Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambao umefikia Zaidi ya asilimia 65 ambao unagharimu Zaidi ya bilioni 3.2.
mkataba wake ni wa mwaka mmoja ambao umeanzia Julai Mosi 2017 na kukamilika Julai mosi, 2018.Hata hivyo Mkandarasi huyo aliomba kuongezewa miezi mitatu ili kukamilisha kazi hiyo na kuzitaja sababu zilizochelewesha mradi huo kuwa ni marekebisho ya michoro,kuchelewa kukabidhiwa mradi na kuongezeka kazi za ziada ikiwemo uzio na barabara.Mkandarasi huyo amesema hivi sasa kinachoendelea ni ujenzi wa zizi,wigo na kazi ya ukamilishaji(finishing).
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa