MAADHIMISHO ya wiki ya Utumishi wa Umma yanatarajia kuanza Juni 16 hadi Juni 23.Katika kufanikisha maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea anawakumbusha watumishi wote kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya mwaka huu.Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo,watendaji na viongozi wa serikali wanatakiwa kujikita katika utoaji wa huduma na kutathimi ubora wa huduma zinazotolewa na kufanya mrejesho wa wateja.
Mkurugenzi pia ameagiza katika maadhimisho hayo kila mtendaji awatembelee watumishi ili waweze kupata fursa ya kutoa mrejesho wa utendaji kazi.Kauli Mbiu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma mwaka 2018 "Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi bora ili kufikia malengo ya Agenda 2063 ya Umoja wa Mataifa na Maendeleo Endelevu"
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa