SHIRIKA la Kanisa katoliki la DONBOSKO Network limetoa vishikwambi 1824 ,kompyuta mpakato 38 na powepoint 19 katika shule kumi za msingi katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Mhasibu wa DONBOSKO padre Celestine Kharkongor amesema vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 885 na kwamba lengo ni kuhakikisha walimu na wanafunzi wanatumia vifaa vya kieletroniki katika tendo la kujifunza na kufundisha na kuleta mapinduzi katika elimu.
Padre Celestine amesema mradi huu unafanyika katika awamu ya pili upande wa Zanzibar na wilaya Songea mkoani Ruvuma,mradi unatekelezwa katika Halmashauri za Manispaa ya Songea na Halmashauri ya wilaya ya Songea.
Amesema DONBOSKO imetoa masanduku 35 yenye vishikwambi 96 kwa kilashule,power point na kompyuta mpakato katika shule za msingi zilizopo kwenye mradi,vifaa vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.575.
Hata hivyo amesema awamu ya kwanza ya mradi huo ilianza mwaka 2017 katika shule za msingi katika mikoa ya Dodoma,Iringa,Dar es salaam,Kilimanjaro na Morogoro.
Kwa upande wake Padre Peter Mutechura ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la DONBOSKO Network Tanzania anayeshughulikia Maendeleo na elimu amesema kupitia program hii mwalimu atatumia vifaa vya kijiditali kama jukwaa la kufundishia na kuifanya wilaya ya Songea kuingia katika mfumo wa kisasa wa kufundishia.
Afisa Elimu Msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Zakia Fandy amelishukuru shirika la DONBOSKO kwa kuanzisha mradi huo katika shule kumi za Manispaa ya Songea ambapo amesema hiyo ni fursa nyingine katika manispaa ya Songea.Hata hivyo amewaagiza walimu wakuu kuhakikisha mradi unatekelezwa kulingana na malengo yaliyowekwa na vifaa hivyo visitumike katika matumizi yasiyostahili.
Nelson Mahenge ni Mratibu wa DONBOSKO Network ambaye ni Mtalaam wa teknolojia ya habari hapa anazungumza program ya kutumia kompyuta,vishikwambi na power point itakavyokuwa inatumika kufundishia ambapo amesema vifaa hivyo vikichajiwa vinaweza kutumika kwa saa zaidi ya nane na kwamba mwalimu anaweza kufundisha hata kama umeme umekatika.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Februari 15,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa