Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imeridhia kuongeza eneo la upandaji miti ya kibiashara kutoka hekari 3905 hadi 20000 ishirini elfu katika Kata ya Mpepo na Liparamba ili kupunguza uteemezi wa misitu ya asili na kuongeza chanzo cha mapato ya serikali.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Dougras Ruambo wakati akiwasilisha taarifa ya upandaji miti ya kibiashara aliyoitoa wakati wa kikao cha kamati ya ushauri cha Wilaya ya Nyasa kilichofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Kepteni John Komba Mbamba-bay Wilayani Nyasa.
Alifafanua kuwa katika Wilaya ya Nyasa kuna miradi miwili ya upandaji miti na miradi hiyo ni wa shamba la Mpepo unaosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na mradi wa upandaji miti wa watu binafsi unaofadhiliwa na Serikali ya Finland kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia mradi wa panda miti kibiashara na lengo la mradi huu ni kutekeleza sera ya misitu ya mwaka 1998 lenye dhumuni la usimamizi wa misitu na upatikanaji endelevu wa mazao na huduma za misitu.
Mkurugenzi Ruambo aliongeza kuwa shamba la miti la Mpepo lina ukubwa wa hekta 3905, katika kuboresha usimamizi shamba limegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni mapera (ipo katika kijiji cha Mtetema) likiwa na ukubwa wa hekta (815) sehemu ya kizota (ipo katika vijiji vya kihulunga, Mtetema na Lunyele) yenye ukubwa wa hekta 2728 na sehemu ya Ndondo ina ukubwa wa hekari 362.
Aliongeza kuwa ili kutimiza ufanisi wa madhumuni ya uanzishwaji shamba na uwekezaji wa Serikali wenye tija, lengo ni kufikia ukubwa wa hekari 20,000 hivyo juhudi kubwa ya pamoja inahitajika ili kufikia malengo haya.
Aidha kwa mwaka wa fedha 2017/2018 serikali kupitia TFS ilitenga fedha na kupanda miti na mpaka sasa jumla ya miti 222,200 sawa na hekta 200, aliitaja miti iliyopandwa ni aina ya misindano, pinusna, pinus, telcunumanii, patula miti hii imepandwa katika kijiji cha sehemu ya mapera iliyopo kijiji cha Mtetema.
Hata hivyo katika mpango kazi wa shamba wa mwaka 2018/2019 TFS imepanga kupanda hekta 300 za miti aina ya misindano (pines). Hekta hizi zipo kijiji cha Mtetema (200) na kijiji cha Mpepo (100) ili kufanikisha mpango huu tayari eneo hili limeandaliwa na hatua ya upandaji zimeanza hivyo upandaji huu utakamilika katika msimu huu wa mvua na hivyo jumla ya hekta 500 za miti ya pine zitakuwa zimepandwa.
Wakala wa huduma za misitu Tanzania kupitia shamba la miti Mpepo umekuwa mstari wa mbele katika kuchangia huduma za jamii katika maeneo yanayozunguka shamba la miti Mpepo. Aliyataja mafanikio hayo kwa ni umeboresha Miundombinu ya barabara na umetoa mabomba rola 17 na bati 60 kwa ajili ya kijiji cha Mtetema na umetoa saruji mifuko 60 kwa ajili ya kijiji cha Kihulunga.
Aliitaja michango mingine ni viriba kilo 40 mbegu za miti kilo 42 aina ya misindano na mikaratusi kwa ajili ya vijiji vya Lunyere, Kihurunga, Mtetema na Mpepo na Wilaya ya Mbinga. Utaalamu wa kuitunza miti hiyo unaendelea na wananchi wanaoishi kuzunguka eneo la upandaji miti wananufaika na ajira
Imeandaliwa na Netho Credo
Afisa Habari Wilaya ya Nyasa
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa