WATOTO zaidi ya 800 wenye umri kati ya miaka 13 hadi 17 wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wamepewa mimba za utotoni katika kipindi cha mwaka 2017/2018.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC wilayani Tunduru,ongezeko kubwa la mimba za utotoni katika wilaya hiyo zimechangiwa na mila na desturi potofu za wakazi wa wilaya hiyo zinazochangiwa na wazazi na walezi.
Ripoti ya kati ya mwaka 2010 hadi 2017 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF linaloshughulikia watoto,inaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya tatu kwa viwango vya juu vya mimba za utotoni baada ya nchi za Uganda na Sudan Kusini.
Kulingana na takwimu hizo za UNICEF,kiwango cha watoto wenye umri chini ya miaka 18,wanaopata mimba za utotoni Sudan Kusini ni asilimia 52,Uganda asilimia 40,Tanzania asilimia 31 na Kenya asilimia 23.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa