Ni wajibu wetu kutambua juhudi za walimu wetu ikiwa pamoja na kupata haki zao za msingi, “ kwahiyo walichokifanya ni wajibu wao.” Hongereni walimu wa Manispaa ya Songea.
Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Songea Devotha Luwungo katika ziara ya kutembelea shule ya Mateka Sekondari na Ruvuma Sekondari iliyofanyika leo 01.02. 2021.
Devotha akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea alisema “mwaka 2020 kama Halmshauri imejitahidi kwasababu haijarudi nyuma kutokana na baadhi ya shule mbili zimepanda ikiwemo shule ya Sekondari Mateka na Ruvuma Sekondari ambapo wanafaunzi wawili wamefanya vizuri zaidi kwa kupata alama ya ufaulu wa daraja la kwanza 1.7 (division 1.7).” Hongereni walimu.
Akiwataja wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne 2020 ambao ulifanyika tarehe 23 novemba 2020, Jackson Kasimu Matembo mwanafunzi wa Mateka Sekondari ambaye amepata daraja la kwanza (division 1.7) na Mwanafunzi Ayubu Mohamed Ayubu mwanafunzi wa Ruvuma Sekondari ambaye amepata daraja la kwanza ( division 1.7).
Naye Mkuu wa shule Mateka Sekondari Melikizedeck Paul Makanja alisema Jackson ni mwanafunzi ambaye alikuwa anajitihada za kujisomea na alikuwa akiongoza darasa toka kidato cha kwanza hadi kidato cha nne kwasababu katika matokeo yake ya kidato cha pili mwaka 2018 alifaulu na kupata daraja la 1.7, pia katika mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2020 mwanafunzi huyo amepata daraja la kwanza (division one) kwa ufaulu wa masomo alama A na B moja ya Kiswahili na C moja ya hesabu.
Makanja alisema Miongoni mwa mikakati ya shule waliyojiwekea kwa mwaka 2020 ilikuwa ni kuhakikisha wanaondoa sifuri 0 ambapo kati ya wanafunzi waliosajiliwa mwaka 2020 walikuwa 66 kati ya hao waliofanya mtihani ni 63 ambao wote wamefaulu ambapo daraja la 1 wamefaulu wanafunzi 6, daraja la pili wamefaulu wanafunzi 16, daraja 3 wamefaulu wanafunzi 14, na daraja la 4 wamefaulu wanafunzi 27 sawa na asilimia 100%. Jackson Kasimu Matembo ni mtoto anayelelewa na bibi yake kwani wazazi wake hawaishi pamoja (walitengana).
Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Ruvuma Altemius Altemius Komba alisema mwanafunzi Ayubu Mohamedi Ayubu ambaye amefaulu na kupata daraja la kwanza kwa kupata alama A - 7 na na alama B moja na C moja. Katika mtihani wake wa kidato cha pili 2018 Ayubu Mohamed Ayubu alifaulu na kupata daraja la kwanza pointi 7 (division 1.7) hivyo matokeo hayo ni halali kuyapata kwani alikuwa akiongoza darasani kila muhula hadi kumaliza kwa masomo yake ya kidato cha nne 2020.
Komba aliongeza kuwa pamoja na matokeo mazuri ya mwananfunzi huyo lakini kuna wanafunzi wengine wawili ambao wamefanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza ambao ni Kelvin Vitalis ambaye amepata ( division 1.10) na mwanafunzi Abdulazak Hamisi Alli ambaye amepata daraja ( division 1.11).
Aliongeza kuwa jumla ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 110, kati ya hao waliofanya mtihani ni 104 na matokeo yao ni daraja la 1 wamefaulu 8, daraja la pili wamefaulu 12, daraja la tatu wamefaulu 12, daraja la nne wamefaulu 58, na waliofeli ni 14. Mikakati waliyojiwekea ili kukabiliana na changamoto ya wanafunzi kufeli mtihani ni pamoja na kuhakikisha kila mwalimu anafundisha mada kikamilifu.
Naye mwanafunzi Ayubu Mohamed Ayubu alisema anafuraha sana kupata matokeo mazuri kama hayo japokuwa alitarajia kupata A katika masomo yake yote lakini hata hivyo anamshukuru mungu kwa hatua aliyofikia. Alisema yeye ni mtoto aliyekosa mzazi mmoja yaani baba ( alifariki 2011) na sasa anaishi na mama yake mzazi ambaye ni mjasiliamali mdogo wa kuuza sweta.
Ndoto za wanafuzi hao kwa baadaye wamesema ni kuwa madaktari.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
01 FEBRUARI 2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa