MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Kanal Ahmed Abbas Ahmed, amewataka wataalamu wa Manispaa ya Songea kuhakikisha wanakamilisha miradi yote iliyoingiziwa fedha ifikapo Desemba 2024. Agizo hilo alilitoa katika ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa hiyo, akilenga kuona maendeleo na kuhimiza utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Kanal Ahmed alitolea mfano wa mradi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea, akipongeza usimamizi mzuri wa kazi. Alisisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi ili wananchi wapate huduma kwa karibu.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Songea, Dkt. Amos Mwenda, alifafanua kuwa mradi wa hospitali ulianza kutekelezwa tarehe 09/12/2021 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 2024. Halmashauri imepokea jumla ya shilingi 2,100,000 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi huo, ikiwa ni katika awamu nne.
Hospitali hiyo ilianza kutoa huduma mnamo tarehe 01/11/2023, ikiwemo huduma za wagonjwa wa nje, maabara, na kliniki ya uzazi na mtoto. Hadi kufikia tarehe 30 Septemba 2024, jumla ya wateja 2,505 walihudumiwa katika kituo hicho.
Ziara hiyo ilifanyika tarehe 23 Oktoba 2024, ikiwa ni sehemu ya kutembelea miradi ya ujenzi wa jengo la mahakama, barabara, na hospitali ya Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa