ALAT ni Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ambayo iliundwa kikatiba mwaka 1984 Disemba na kuanza kutumika rasmi mwaka 1985 kwa lengo la kupigania haki za Halmashauri na kuwa sauti moja katika kuleta maendeleo ya Halmashauri husika,
Katika kutekeleza lengo hilo, wajumbe wa ALAT Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Kelvin Mapunda wamefanikiwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji Mbinga iliyoanza tarehe 07 hadi 08 Disemba 2023.
Mhe. Kelvin amewapongeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote Mkoani Ruvuma kwa kusimamia na kuratibu vizuri miradi ya maendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa katika Halmashauri.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa jengo la Zahanati ya kijiji cha Tukuzi ambayo imejengwa kwa jumla thamani ya Mil. 49,925,000 ambapo kati ya fedha hizo nguvu za wananchi kiasi cha Mil. 12,800,000, pia Mil. 27,875,000 fedha kutoka chama cha ushirika pamoja na shilingi 9,250,000 fedha kutoka mfuko wa jimbo.
Mradi wa kikundi cha VIJANA KAZI MHEKELA ambao walipata mkopo kutoka Halmaashauri wa (10%) wenye jumla ya shilingi 24,000,000 ambapo wanajishughulisha na shughuli ya ufyatuaji wa tofari za saruji ambacho kilianzishwa tarehe 27 Julai 2022 kikiwa na wanachama 8 ambapo hadi hivi sasa wamefanikiwa kujiajri na kuajiri vijana 12 ambapo kati ya hao wanaume 10, na wanawake ni 2 pia walitembelea kiwanda cha Kahawa Mbinga.

Ziara hiyo itakamilika tarehe 08 Disemba ambapo watatembelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
ALAT RUVUMA
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa