Na;
Amina Pilly;
Mwandishi ALAT
Mkoani Ruvuma.
ALAT ni chombo kinachosaidia kukuza maendeleo ya Serikali za mitaa zilizo huru na kutoa mchango katika kupeleka madaraka kwa wananchi, kuwasaidia madiwani, Mameya na wenyeviti katika majukumu yao kama wawakilishi waliochaguliwa kidemokrasia pamoja na kutoa uongozi, kuhimiza, kukuza ufanisi, uhuru,uwajibikaji, uwazi na demokrasia kwenye mfumo wa Serikali za Mitaa Tanzania na kwingineko duniani.
Katika kutekeleza majukumu hayo, Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mbinga Kelvin Mapunda ameongoza kamati hiyo katika kutembelea miradi mabalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmshauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma iliyofanyika jana tarehe 31 Mei 2022.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na ALAT Mkoa wa Ruvuma ni pamoja na ujenzi wa Sekondari ya Wasichana Namtumbo inayogharimu shilingi bil.3 tatu inayojengwa katika kijiji cha Migelegele ambayo pia ilianza kujengwa tarehe 06 Aprili ambapo ujenzi huo unatarajia kukamilika 29 juni 2022 pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Namtumbo uliogharimu kiasi cha shilingi Mil.500 ambao ulitakiwa kukamilika 30 Machi 2022.
Mheshimiwa Mapunda alisema kikao hicho kilitakiwa kufanyika tarehe 28 Februari 2022 lakini kutokana na muingiliano wa kazi za Serikali hakikuweza kufanyika badala yake kimefanyika jana 31 Mei 2022 kilichoshirikisha Wakurugenzi wa Halmashauri zote na wenyeviti wa Halmashauri, Madiwani na Mstahiki Meya.
Alisema lengo kuu la kufanya ziara ya kutembelea miradi ya ni kuleta mshikamano baina ya Halmashauri na Halmashauri nyingine pamoja na kujengeana uzoefu wa kiutendaji katika kusimamia na kutekeleza miradi ya Maendeleo.
Amewarai Madiwani wote Mkoani Ruvuma kuhakikisha wanashirikiana na wataalamu katika kusimamia kwa ufanisi miradi yote inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita na hatapenda kusikia kama kuna Halmashauri ambayo ipo chini katika utekelezaji wa shughuli za Serikali. Alisisitiza.
Alibainisha kuwa tarehe 27 Juni 2022 ALAT Mkoa wa Ruvuma imepanga kutembelea Mkoa wa Tanga kwa lengo la kwenda kujifunza mpangilio wa Mji, Uwekezaji wa Utalii, kuijifunza namna walivyofanikiwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo na kilimo cha matunda (Machungwa). Hivyo amewataka Wakurugenzi wote kila Halmashauri kuhakikisha wanawagharamia wajumbe wote wa kamati ya ALAT kuelekea Mkoani Tanga.
Nao Madiwani wakipaza sauti zao wakihoji kuhusu stahiki zao ambapo alisema nanukuu” Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wabunge, Madiwani huongoza kwa muda wa miaka 5 tano sawa na miezi 60 sitini lakini 2020 uongozi ulikoma tarehe 30 juni 20220 badala ya kukoma mwezi Disemba 2020 ambapo katika maslahi yao walilipwa stahiki za miaka 4 nne na miezi sita 6 ambapo ni tofauti ya miaka mingine ya nyuma, hivyo waliomba uongozi wa ALAT Mkoa wa Ruvuma kufikisha lalamiko lao ngazi ya juu na kupatiwa ufumbuzi pamoja na kuongezewa maslahi yao.”Mwisho wa kunukuu”
Naye Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano alisema ni kweli kwa upande wa Manispaa ya Songea mara baada ya kuingia madarakani alipokea lalamiko hilo kutoka kwa Waheshimiwa Madiwani waliokoma uongozi mwaka 2020 na aliomba uongozi wa ALAT Mkoa wa Ruvuma kutatua changamoto hiyo ili madiwani hao waweze kulipwa stahiki zao za miezi sita iliyobaki kipindi cha uongozi huo.
Mbano alitoa rai kwa Wajumbe wa ALAT Mkoa wa Ruvuma kuisaidia timu ya Majimaji kwa kuichangia hisa ili kuweza kuipandisha daraja kwakuwa Timu hiyo imekuwa ikiwakilisha Mkoa wa Ruvuma ambapo kwasasa imekosa walezi wakuifadhili timu hiyo ambapo mpango rafiki uliowekwa wa kuisaidia timu hiyo ni kubadili mfumo wa uendeshaji uliopo na kuibinafsisha kwa kuisajili kampuni ili kuleta tija katika michezo.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa