Mwenyekiti ALAT Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kelvin Mapunda amewataka Madiwani wote Mkoani Ruvuma kuendelea kushirikiana na Wataalamu wa Halmashauri katika kusimamia na kutekeleza ujenzi miradi ya Maendeleo.
Alisema Kila Halmashauri inatakiwa kusimamia na kukusanya mapato ya ndani ili Halmashauri iweze kufanikisha katika ukusanyaji wa mapato na kufikia lengo lililokusudiwa.
Hayo yamejiri wakati wa ziara ya ALAT Mkoa wa Ruvuma iliyofanyika kuanzia tarehe 04 hadi 05 Oktoba 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa lengo la kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Halmashauri hiyo.
Mhe. Kelvin ametoa Rai kwa Wataalamu wa Halmashauri Mkoani Ruvuma kusimamia zoezi la utaoji wa chakula kwa wanafunzi shuleni ambao utawezesha upatikanaji wa lishe bora na ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Litumbandyosi kilichojengwa kwa gharama ya shilingi Mil. 599,013,700 ambacho kipo katika hatua ya ukamilishaji, pamoja na mradi wa kikundi cha MWO ( Mbalawala Woman Organization) ambacho kinajishughulisha na kiwanda cha utengenezaji nishati mbadala ya makaa yam awe ya kupikia, utunzaji wa mazingira, kilimo, uwezeshaji kijamii, na huduma za chakula na usafi wa mazingira katika migodi ya makaa yam awe ya ngaka.
Kwa upande wake Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Amandus Chilumba amezitaka Halmashauri zote Mkoani Ruvuma kuendelea kuwa wabunifu wa vyanzo vya mapato katika Halmashauri ili ziweze kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato ya Serikali. “Alisisiiza”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
ALAT- RUVUMA,
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa