MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Ruvuma amefanya operesheni ya kushitukiza katika viunga vya Mji wa Songea na kufanikiwa kumkamata Mfanyabiashara mmoja ambaye alikuwa ameficha mafuta ya kula ambapo Mndeme alimkabidhi Mfanyabiashara huyo kwa Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma ili kumchukulia hatua za kisheria.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema katika Mkoa wa Ruvuma bidhaa za mafuta,sukari na vyakula vingine zipo za kutosha ambapo ametoa rai kwa wafanyabiashara kuhakikisha wanauza bidhaa hizo kulingana na bei ya soko ili kutowakomoa waumini wa dini ya kiislamu ambao wanaanza mfungo wa Ramadhani.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa