1. Tulipitisha uamuzi wa kuunganisha mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kuiboresha Sekta ya Hifadhi ya Jamii na pia ni moja ya ombi la vyama vya wafanyakazi.
2. Wakati tunaingia madarakani tulikuta deni la Shilingi Tril. 1.2 kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, lakini hadi kufikia machi 2017 tulimaliza kulipa deni lote.
3. Agosti 1, 2018 idadi ya wastaafu walikuwa 8000 ambao walikuwa wanadai jumla ya bilioni 740 ambapo bilioni 550 zimeshalipwa na natumaini kabla ya Januari 2019 zitalipwa zote ziishe.
4. Naitaka Mifuko iboreshe daftari la wastaafu ili kuondoa wastaafu hewa na wale waliosajiliwa mara mbili.
5. Mifuko ya hifadhi ya jamii nawasisitiza mpunguze matumizi yasiyo ya lazima.
6. Mifuko ya hifadhi ya jamii punguzeni gharama zisizo za lazima za uendeshaji wa mifuko, kwa sasa mifuko ipo miwili tu hakuna haja ya kushindana.
7. Niwakati wa kuwapa ‘motivation’ wafanyakazi na si kuwa ‘discourage’ fomula nzuri ni ile ya kuwasaidia wafanyakazi.
8. Nimeamua angalau tuwe na kipindi cha mpito, kikokotoo kilichokuwa kinatumika katika kila mfuko kabla ya kuunganishwa kiendelee hadi mwaka 2023.
9. Tunataka mifuko hii iwasaidie wafanyakazi, ninawapenda sana wafanyakazi na nitaendelea kuwapenda.
Idara ya Habari- MAELEZO
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa