UTAFITI wa nne uliofanyika katika ngazi ya kaya kuanzia Oktoba 2016 hadi Agosti 2017 ulibainisha kuwa wastani wa kitaifa wa maambukizi ya VVU kwa watu wenye umri wa miaka 15 hadi 49 ni asilimia 4.7. Wanawake ni asilimia 6.2 na wanaume ni asilimia 3.1.
Nchi yetu imeridhia na kuanza utekelezaji wa kauli mbiu ya kidunia ya ifikapo 2020 ya asilimia 90 ya watu wanaoishi na VVU wawe wamejua hali zao za maambukizo,asilimia 90 ya waliopimwa VVU na kugundulika kuwa wana maambukizo wapatiwe dawa za kufubaza makali ya VVU na asilimia 90 ya watu wanaotumia dawa wawe wamefubaza VVU.
Nchini Tanzania ni asilimia 52.2 tu ya wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 – 64 ndiyo walitoa taarifa kuwa wanaojua hali zao za maambukizo ya VVU ambapo Wanawake ni asilimia 55.9 na Wanaume ni asilimia 45.3
Kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 – 64 ambao wanajua hali zao za maambukizo ni asilimia 90.9 ndiyo walitoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU kati yao Wanawake ni asilimia 92.9 na Wanaume ni asilimia 86.1.
Kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 – 64 ambao wametoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU,asilimia 87.7 ya watu hao inaonesha kiasi cha VVU kimefubazwa,kati yao Wanawake ni asilimia 89.2 na Wanaume ni asilimia 84.
Hivyo basi, Kulingana na utafiti huo Tanzania inafanya vizuri,hata hivyo lakini tatizo kubwa ni katika kufikia 90 ya kwanza, kwa kuwa ni asilimia 52.2 tu ya wenye VVU wanajua hali zao. Tatizo hili ni kubwa zaidi miongoni mwa wanaume, kwa sababu ni asilimia 45.3 tu ya wanaume wanaoishi na VVU wanajua hali zao.
Madhumini ya kampeni hii ni kufikia malengo ya Tanzania kwamba ifikapo mwaka 2020 asilimia 90 ya watu wanaoishi na VVU wawe wanatambua hali zao za maambukizi, asilimia 90 kati yao wanatumia ARV na asilimia 90 ya wanaotumia ARV kiwango chao cha VVU mwilini kinashuka.
Malengo ya kampeni ni kusaidia kutimiza malengo ya Tisini tatu (90 90 90) kwa kuzingatia malengo yaliyowekwa Kitaifa na Mikoa.
Mikoa ya utekelezaji wa mradi wa Tulonge Afya (Upande wa Uhamasishaji) na Boresha Afya (Upande wa Utoaji wa Huduma) ni Arusha, Kagera, Geita, Shinyanga, Kigoma,Mara,Mwanza,Tabora, Singida, Iringa, Njombe, Mtwara, Morogoro, Lindi, Ruvuma, Dodoma Kilimanjaro, Manyara na Simiyu.
Walengwa wa kampeni hii ni Watu ambao hawajawahi kupima VVU na wako katika hatari ya kumbukizwa au kuambukiza VVU:
Wanaume wenye Umri chini ya Miaka 45,Wasichana walio katika umri wa balehe,Wanawake wenye umri wa miaka 15-24,Akinamama wajawazito,Watu ambao wameambukizwa VVU na hawajaanza kutumia ARV na Akina Mama wanaoishi na VVU na Wananyonyesha na watoto wao.
Njia za Mawasiliano ambazo zinatumika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni ,Radio za Kitaifa,Radio za mikoa au kijamii,mitandao ya kijamii,televisheni,watoa huduma za Afya na walielimisharika,mawasiliano ya ana kwa ana,Machapisho ya aina mbalimbali na Mikutano ya ulaghabishi kitaifa,mikoa na wilaya.
Makala imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari serikalini
Juni 20,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa