Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiwa katika ufunguzi wa Semina ya RITA Kwa Viongozi wa Wilaya na Mkoa wa RUVUMA inayoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea kuanzia hapo jana 03/03- 04/03/2020.
RITA ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Katiba na Sheria yenye Majukumu , pamoja na kusimamia na kuratibu Usajili wa Vizazi na Vifo Tanzania Bara. Lengo kuu la RITA ni kuhakikisha kila mtoto wa umri chini ya miaka mitano anasajiliwa na kupata cheti cha kuzaliwa na kumpa mtoto haki yake ya msingi ya kutambuliwa.
Mndeme alisema, Historia ya Usajiili imeanza miaka mingi hata kabla ya Uhuru na Usajili ni hatua inayomwezesha mwananchi kuweza kutambuliwa na kusajiliwa taarifa zake kuingizwa kwenye Mfumo Rasmi wa Serikali ambao ni Daftari za kusajili Mfumo.
Alisema “Maisha ya Binadamu yanaanza pale tu anapozaliwa kwa hiyo lazima tufahamu Mkakati wa Serikali kusajili Watoto Chini ya Miaka Mitano ambapo Kundi hilo ni la Kimkakati na nikipaumbele.Hivyo Takwimu za Vizazi ni Kichocheo cha Maendeleo Nchini kwani Serikali hupanga matumizi ya Maendeleo ya Muda mfupi na Muda mrefu na Mipango hiyo ya Serikali huanzia Halmashauri, na bila Takwimu huwezi kupata mahitaji muhimu naya Msingi hususani; Takwimu za Madawati kwa shule za Msingi, pia alisema huduma hiyo itatolewa bure bila malipo”. Alisisitiza.
Alibainisha changamoto mbalimbali zilizopelekea kukwamisha ufanisi wa zoezi hilo ni pamoja na Umbali, Wazazi/ Walezi Kushindwa kulipia gharama, pamoja na uelewa mdogo wa Usajili wa Watoto. Alisema Ili kutatua changamoto hiyo, Huduma hiyo sasa itatolewa kwenye ofisi za Kata/ Vijiji/ Mtaa bila malipo yoyote nani zoezi endelevu sio kampeni. Mradi huu umeanza kutekelezwa katika mikoa Mbeya, Songwe, Iringa, Geita, Shinyanga, Lindi, Mtwara, Mara, Simiyu, Dodoma, Singida ,Morogoro, na Pwani na sasa tunajiandaa na utekelezaji katika Mkoa wa Ruvuma.
Hakusita kuwaondoa hofu wananchi wa Mkoa Wa Ruvuma juu ya Ugonjwa hatari wa Korona ambao ni tishio Duniani kote. Alisema “ hadi sasa Mkoa wa Ruvuma hakuna mgonjwa Yeyote aliyeripotiwa kuuguwa au kugundulika kuwa na virus vya ugonjwa hatari wa korona ambapo, amewaasa wananchi wote Mkoani Ruvuma kuchukua Tahadhari mapema kwa kuacha tabia/desturi ya kusalimiana kwa kupeana mikono,kukumbatiana, kuacha kunawa maji katika chombo kimoja,kuacha kukohoa/ kupiga chafya bila kukinga kitambaa au mikono ili kuzuwia maambukizi yasiweze kutokea, pia Serikali imejiandaa kwa kutenga kituo/chumba maalmu kama hospital au kituo cha afya kwa ajili ya kupokea wagonjwa mara tu itakapotokea.”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa