TATIZO la ukataji wa miti na misitu hovyo limesababisha nchi yetu kuwa na zaidi ya asilimia 60 ya eneo lililoathiriwa na jangwa kwa kuwa vyanzo vingi vya maji vimeendelea kukauka mwaka hadi mwaka.Takwimu zinaonesha kuwa nchi yetu kila baada ya wastani wa miaka minne kunatokea ukame na kuathiri karibu watu milioni 3.6 katika Sehemu za Dodoma, Singida, Shinyanga, Mwanza na Mara.
kutokana na ukataji wa misitu, kilimo kisicho cha kitaalam kumesababisha mmomonyoko wa ardhi na kusababisha udongo kupoteza rutuba na hivyo kusababisha ukosefu wa mvua na mafuriko ambayo huwaathiri wananchi kila mwaka.Uharibifu wa mazingira nchini sio unaleta athari katika ardhi na maji tu lakini pia unachafua hewa na kusababisha madhara makubwa kwa afya ya wanadamu na viumbe vingine hai ambavyo hutegemea hewa safi ili viweze kuendelea kuishi.
Hali halisi inayoendelea hivi sasa inathibitisha kuwa taasisi zinazoshughulikia mazingira zimeshindwa kuzuia uharibifu wa mazingira licha ya kuwepo sera na sheria matokeo yake watanzania wengi wanapata athari za kiafya na kimazingira hali hii ni mbaya kwa kuwa siku moja tunaweza kuangamia sote.
Kutokana na uchafuzi huo wa mazingira historia inaonesha kutoka mwaka 1980 hadi 2015 mafuriko nchini mwetu yameshatokea mara nyingi na kusababisha vifo vya watu na wengine kuathiriwa vibaya katika makazi yao hasa katika Sehemu za Tanga,Dar es salaam, Mbeya, Zanzibar, pemba,Geita,Shinyanga, Pwani, Morogoro, Arusha, Rukwa, Iringa, Kigoma,Lindi na Dodoma.
Sheria zipo kinachotakiwa ni kuhakikisha sheria hizo zinachukua nafasi yake kwa wale wote watakaobainika kwenda kinyume na sheria za mazingira ukiwemo ukataji wa misitu na uchafuzi wa vyanzo vya maji.Tusipoangalia vita kuu ya tatu ya Dunia ambayo itasababishwa na uchafuzi na uharibifu wa mazingira inakuja ambayo italeta maangamizi makubwa kwa viumbehai wakiwa binadamu.
Mwandishi wa makala haya ni Albano Midelo.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa