Askofu wa Jimbo la Mbinga Mhashamu John Ndimbo amewataka Waumini kumtegemea Mungu ili waweze kuwa na maendeleo ya kimwili na kiroho na kuepukana na kutegemea nguvu za giza ambazo huleta woga na umaskini.
Ameyasema hayo wakati akihubiri Misa takatifu katika kanisa la Mtakatifu Bikira Maria msaada wa wakristo Parokia ya Makwaya Jimbo Katoliki la Mbinga katika sherehe za parokia hiyo kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Askofu ndimbo amesisitiza kuwa ili jamii iweze kuwa na maendeleo inatakiwa kumtegemea mungu kwa kuwa katika kumtegemea kinakupa maarifa yatakayokuwezesha kupambana na umaskini na kuwa na maendeleo ya kimwili na kiroho.
“ Epukeni kabisa kutegemea nguvu za giza ambazo zitakufanya uwe masikini na woga wakati wote na kamwe jamii inayotegemea nguvu za giza haiwezi kuwa na maendeleo’’,anasisitiza Askofu Ndimbo.
Hata hivyo Mhashamu Ndimbo ameipongeza jamii ya watu wa parokia ya Makwaya kuwa wanamaendeleo na wamefikia mahali ambapo wamepiga hatua nyingi za kichumi ambazo ni wana Mtandao wa maji uliotengenezwa na kanisa,Wana Zahanati inayohudumia wakazi wake na wanakanisa zuri lililojengwa kwa ushirikiano wao.
“ Jamii inyotegemea nguvu za giza kamwe haiwezi kuwa na maendeleo kwa kuwa muda wote inakuwa na uoga ambao unasababisha kutokuwa na maendeleo na kubaki kuwa maskini muda wote’’,amesema.
Katika hatua nyingine Askofu Ndimbo alimpongeza mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mbunge wa Jimbo la Nyasa Ambaye pia na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya kwa kuwahamasisha wananchi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili waweze kuondokana na umaskini.
Kanisa katoliki la Mtakatifu Bikira Maria msaada kwa wakristo lilianzishwa mwaka 1968 na kufikia kilele cha miaka 50 mwaka huu 2018 .
Imeandaliwa na Netho Credo
Afisa Habari Wilaya ya Nyasa
Oktoba 19,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa